HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Yaamrisha Mwanahabari Jacque Maribe Afanyiwa Uchunguzi Wa Kiakili.

Mahakama ya milimani jijini Nairobi  imetoa agizo la kupelekwa kwa uchunguzi wa kiakili kwa mwanahabari Jacque Maribe kabla yakujibu mashtaka ya mauaji dhidi yake.

Agizo hilo limejiri baada ya upande wa mashtaka kuiomba mahakama kuwapatia muda wakumfanyia uchunguzi wa kiakili Maribe kabla ya kusomewa mashtaka dhidi yake.

Ombi ambalo limepingwa na wakili wa mshukiwa huyo Katwa Kigen ambaye amependekeza mteja wake asomewe mashtaka kwanza kabla ya kufanyiwa vipimo hivyo lakini mahakama imepinga na kuagiza apelekwe kwa vipimo hivyo.

Wakati huo huo wakili Cliff Ombeta wa Joseph Irungu ambaye ni mshukiwa wa pili katika kesi hio ya mauji ya Monica Kimani ameidokezea mahakama mteja wake hajakua akipokea matibabu ambayo alitakiwa kuyapata kama ilivyoagizwa na mahakama hapo awali.

Kufikishwa mahakamani kwa wawili hao kunajiri baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji kuagiza wawili hao wafunguliwe mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani

Show More

Related Articles