People Daily

Swala La Umiriki Wa Ardhi La Zidi Kuwa Donda Sugu Kwa Wakaazi Wa Kwale.

Zaidi ya familia 20 katika kijiji cha mbele  gatuzi dogo la kinango kaunti ya kwale  wanaishi kwa hofu ya  kufurushwa  katika kipande chao cha ardhi   cha takriban  ekari 1000 licha ya kudai  kuishi katika ardhi hio kwa zaidi ya miaka 100 .

Wakaazi hao wanasema Chaka Nyamawi  aliye  naibu kamishna kaunti ya  Tanariver  anadai kumiliki ardhi hio na  kuwaka  wakaazi  wanaoishi  katika ardhi hio  kuhama ili kumpatia nafasi ya kuendeleza shughuli zake .

Aidha waakazi hao wanaitaka  serikali  ya kaunti  na ile ya kitaifa  kuingilia kati mzozo huo na kutoa mwafaka  kabla ya  hali hio haijahujumu usalama kati ya pande hizo mbili.

Haya yanajiri huku maswala ya umiliki wa ardhi kwale  yakisalia kuwa donda sugu hata licha ya serikali kulivalia njuga swala zima la umiliki wa ardhi eneo la pwani .

Show More

Related Articles