HabariPilipili FmPilipili FM News

Kenya Yapokea Ufadhili Wa Millioni 24 Kutoka Kwa Muungano Wa Mataifa EU.

Kenya imethibitidsha kupokea EURO elfu 215 ambazo ni sawa na shilingi milioni 24 kutoka muungano wa mataifa ya ulaya eu, kama sehemu ya ufadhili wa kongamano la kiuchumi almaarufu Blue Economy linalo tarajiwa kufanyika humu nchini mwezi ujao wa novemba.

Katibu katka wizara ya mambo ya nje Macharia kamau ,amesema pesa hizo ambazo ni zaidi ya robo ya bajeti ya kuandaa mkutano huo wa kimataifa, ni sehemu tu ya msaada wa kifedha wanaotarajia kutoka kwa wafadhili.

Aidha umoja wa ulaya EU pia umethibitisha kutoa ufadhili huo kwa ajili ya kongamano hilo litakaloandaliwa kuanzia novemba 26 hadi 28 jijini Nairobi mwaka huu

Kenya atakua mwenyeji wa mkutano huo kwa ushirikiano na Canada , ikiwa sehemu ya mipango ya  taifa kushirikisdha washikadau mbalimbali jinsi ya kufaidi na raslimali ya bahari, maziwa pamoja na mito ambazo kwa pamoja yanafahamika kama Blue economy.

Show More

Related Articles