HabariMilele FmSwahili

Joseph Irungu na Jacque Maribe kusalia rumande hadi tarehe 15 Oktoba

Joseph Irungu almaarufu Jowie na mtangazaji Jacque Maribe wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji watasalia rumande hadi jumatatu ijayo. Jaji wa mahakama kuu Jessi Lessit ameamuru Joseph Irungu kupokea matibabu kutokana na jeraha la risasi kabla ya kupelekwa katika gereza la Industrial Area. Naye Maribe atafanyiwa uchunguzi wa kiakili katika hospitali ya Mathare.Wawili hao watarejea mahakamani Oktoba 15 kujibu au kukana mashtaka ya kumuua Monica Kimani.

Show More

Related Articles