HabariMilele FmSwahili

Wazazi walaumiwa kwa visa vya ununuzi wa karatasi gushi za KCPE na KCSE

Serikali inasisitiza wazazi ndio wa kulaumiwa kwa visa vya ununuzi wa karatasi gushi za mitihani ya kitaifa KCPE na KCSE inavyoshuhudiwa wakati huu.Mwenyekiti wa baraza la mtihani George Magoha anasema hadi asubuhi ya leo,wamepokea visa kadhaa vya wazazi kuhadaiwa na matapeli kuwapa watoto wao wanaofanya mitihani mwaka huu pesa ili kununua karatasi hizo ambazo ni gushi.Akiongea kwenye mkao uliowaleta pamoja wadau wa elimu kuweka mikakati jinsi ya kufanikisha mitihani hiyo,Magoha anasema huenda wakalazimika kuwakamata wazazi wanaowapa wanao pesa kununua karatasi hizo.Ni usemi unaoridhiwa na katibu katika wizara ya elimu Bellio kKipsang’ anayesema serikali sasa itawalenga wazazi wanaojihusisha na uovu huo akisema unatishia kuathiri mitihani ya mwaka huu.

Show More

Related Articles