HabariMilele FmSwahili

Mamake Sharon Otieno aitaka mahakama kumnyima dhamana Obado

Mamake Sharon Otieno anayedaiwa kuuwawa na gavana wa Migori Okoth Obado amewasilisha ombi katika mahakama kuu akitaka gavana Obado kunyimwa dhamana.Melinda Auma anasema iwapo Obado ataachiliwa kwa dhamana huenda akatatiza uchunguzi.Wakati huo huo,mahakama kuu itaamua Ijumaa hii iwapo itawaachilia kwa dhamana gavana Obado,msaidizi wake Michael Oyamo na karani wa kaunti Caspel Obiero.Ni baada ya kujumilishwa kesi zao za mauaji ya Sharon.Jessie Lessit ni jaji wa mahakama kuu.Wakati huo mahakama imepokea ombi la kujumuishwa katika kesi hiyo shirikisho la mawakili kinamama  fida.

Show More

Related Articles