HabariMilele FmSwahili

Kampeni ya useneta Migori yaingia kipindi cha lala salama uchaguzi ukitarajiwa jumatatu ijayo

Kampeni ya kiti cha usetena kaunti ya Migori imeingia kipindi cha lala salama leo uchaguzi mdogo ukitarajiwa jumatatu ijayo. Kinara wa ODM Raila Odinga jana alifungua sakafu ya kampeni hiyo akimpigia debe, muaniaji wa ODM Dakta Ochilo Ayacko. Kiti hicho kimewavutia wawanaiji 6 aidha macho yote yanaelekezwa kwa Ayacko na mpinzani wake wa karibu, Eddy Gicheru Oketch anayewania wadhifa huo kwa hisani ya chama cha Federal Party of Kenya. Aidha wito kuimarishwa usalama umetolewa kipindi hiki cha kampeni na siku ya uchaguzi, wenyeji wakiomba utulivu kipindi hicho.Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa seneta Ben Olouch mwezi Juni baada ya kuugua saratani.

Show More

Related Articles