HabariMilele FmSwahili

Walimu nchini wakongamana Busia kuhudhuria maadhimishi ya siku ya walimu duniani

Walimu nchini wanakongamana wakati huu katika shule ya msingi ya Amagoro huko Teso kaunti ya Busia kuhudhuria maadhimishi ya siku ya walimu duniani. Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion anatarajiwa kutumia mkutano huo kueleza chanzo cha kutibuka mazungumzo yalioandaliwa mjini Naivasha kusaka mwafaka na tume ya kuwaajiri walimu TSC. KNUT pia itatumia mkutano huu kushinikiza TSC kusitisha uhamisho wa walimu na kupandishwa vyeo walimu elfu 40.

Show More

Related Articles