MichezoPilipili FmPilipili FM News

Bunge La Kilifi Lahimizwa Kupitisha Mswada Wa Kufadhili Michezo.

Wito umetolewa kwa bunge la Kaunti ya Kilifi kupitisha mswada unaolenga kuzifadhili timu zote zinazoshiriki katika Ligi ya kitaifa ya National Super League hapa Pwani.

Hatua hii inajiri baada ya kubainika kuwa timu nyingi zinazoshiriki ligi hio Kaunti ya Kilifi zimekuwa zikikumbwa na changamoto kuu  yakifedha pamoja na vifaa mhimu vya wachezaji.

Akitoa wito huo mjini Kilifi, mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya anasema hatua ya  kupitishwa kwa mswada huo kutatoa fursa ya  kutambua na kukuza vipaji vya wachezaji.

Anasema hatua hio aidha  inalenga kuwapa motisha zaidi vijana hivyo kuwaepusha kutokana na janga la mihadharati na itikadi kali ambapo vijana wengi  hapa Pwani wamekuwa wakihusishwa navyo.

 

Show More

Related Articles