HabariPilipili FmPilipili FM News

Melania Trump Awasili Nchini.

Mkewe rais wa marekani Donald Trump Melania Trump tayari amewasili humu nchini ikiwa ni siku yake ya nne leo katika ziara yake barani afrika kufadhili miradi ya afya na elimu.

Melania Trump aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta majira ya saa tatu usiku.

Melania ambaye ni mara yake ya kwanza kuzuru taifa hili, hii leo anatarajiwa kufanya mazungumzo ya kina na mama wa taifa Mageret Kenyatta.

Tayari amekamilisha ziara yake katika nchi za Malawi na Ghana na baada ya kenya anatarajiwa kukamilisha ziara yake ya Afrika nchini Misri.

Show More

Related Articles