HabariMilele FmSwahili

KNUT yatishia kugoma iwapo TSC haitaandaa majadiliano ya kuafikiana

Chama cha KNUT kimeipa tume ya kuwaajiri walimu wiki mbili kuandaa majadiliano ya kuafikiana lau sivyo watashiriki mgomo.Wakizungumza baada ya kusambaratika mazungumzo baina yao na muajiri wao TSC, KNUT kupitia katibu Wilson Sossion, inatuhumu TSC kwa kukosa nia njema kwenye majadiliano hayo.Sossion ameshtumu hatua ya TSC kukatalia mbali ombi lao kutaka walimu 85 waliokuwa wamehamishwa shule zingine kurejeshwa shule walizofunza awali.Katika taarifa hata hivyo Sossion anasema wako tayari kuendelea na majadiliano hayo kutafuta mwafaka sio tu kuhusu suala hilo bali pia, mkataba wa makubaliano ya pamoja yaani CBA, uhamisho wa walimu, mfumo wa tathmini ya utendakazi wa walimu pamoja na mpangilio wa kuwapandisha daraja

Show More

Related Articles