HabariMilele FmSwahili

Raila asisitiza kufanyiwa marekebisho katiba

Kinara wa ODM Raila Odinga anasema lazima katiba ifanyiwe marekebisho.Akizungumza huko Migori ambako anampigia debe mgombea wa useneta wa ODM kwenye nyanganyiro cha tarehe jumatatu ijayo, Raila anasema wakenya ni lazima washirikishwe kwenye kura ya maoni kufanyia marekebisho katiba hii iliyoidhinishwa mwaka wa 2010.Amesisitiza kuwa hakuna aliye na uwezo wa kuzuia wazo hilo kwani tayari wakenya wanakubaliana kwa kauli moja katiba ya sasa imekuwa mzigo mkubwa kwao.

Show More

Related Articles