HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu Elfu 43,773 Pekee Ndio Hutumia Dawa Za Kupunguza Makali Ya HIV Mombasa.

Watu 43, 773 pekee wenye virusi vya HIV Kaunti ya Mombasa ndio wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo ARV’s , kati ya idadi kamili ya wathiriwa ambayo ni 95, 310 takwimu ambayo ni ya tangu januari mwaka jana hadi sasa.

Wengi wanaotumia dawa hizo ni wanawake ambao kwa ujumla ni 28, 520 ikilinganishwa na wanaume ambao ni 14, 196.

Haya nikulingana na Zaitun Ahmed Mshirikishi mkuu wa kitengo cha afya kinachoshughulikia maradhi hayo kaunti ya Mombasa.

Zaitun anasema huenda idadi hiyo ya wanawake imechangiwa na kinamama wajawazito ambao hulazimika kupimwa virusi hivyo, na mara nyingi wanapopatikana wameathiriwa hulazimika kutumia dawa za ARV’s.

 

Takwimu hiyo aidha imefichua  kuwa jumla ya watoto 700 wa kati ya miaka 10 – 14 wanatumia dawa hizo, umri wa kati 15 – 19 ikiwa ni watu 900, huku umri wa kati ya miaka 20 – 24 ikiwa ni wathiriwa 1,385, na wenye umri wa miaka 25 na zaidi wakiwa ni 31,340.

Show More

Related Articles