HabariPilipili FmPilipili FM News

Imebainika Wanawake Ndio Hununua Sana Dawa Za Upangaji Uzazi Kuliko wanaume.

Imebainika kuwa wateja wengi Kaunti ya Mombasa wanaonunua dawa za kupanga  uzazi  yaani Contraceptives  kwenye maduka ya kuuza dawa hizo ni wa kike.

Wengi wao wenye umri wa kati ya miaka 20 – 35 hupendelea kutumia tembe za Femi Plan ambazo huanza kutumiwa siku tano baada ya kipindi cha hedhi.

Hata hivyo licha ya kuwapo kwa mipira ya kondomu ya jinsia zote , na ambayo pia hutumika kwa upangaji uzazi, wanawake wamekuwa wakiwanunulia waume mipira hiyo kwa kile kinachotajwa wanaume wengi kuogopa.

 

Show More

Related Articles