HabariPilipili FmPilipili FM News

Utumiaji Wa Mipira Ya Kondomu Wapingwa Na Viongozi Wa Dini.

Katibu mkuu wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Sheikh Mohamed Khalifa amekuwa wa hivi karibuni kuipinga vikali utumiaji wa mipira ya kondomu kama njia moja wapo ya kupunguza mambukizi ya virusi vya HIV.

Khalifa anasema japo hatua hiyo inatajwa kuhakikisha wanaoshiriki tendo la ndoa wako salama, suala hilo ni kinyume na sheria ya dini ya kislamu.

Sheikh Khalifa anahisi utumizi wa mipira hiyo ni moja wapo ya njia ya kuwahamasisha watu kundelea kumuasi mwenyezi Mungu na kuendelea kupotoka kimaadili.

Show More

Related Articles