HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Watishia Kugoma.

Huenda walimu wakaendelea na shinikizo zao za kufanya mgomo baada ya Mazungumzo baina yao na tume ya kuajiri walimu nchini TSC kukosa kuzaa matunda.

Maafisa kutoka pande zote mbili walikosa kuafikiana katika mkutano, ulioandaliwa Naivasha siku ya Jumatano, ambapo TSC ilikataa kutekeleza ombi la chama cha walimu KNUT la kutaka uhamisho wa walimu wakuu 85, ambao pia ni maafisa wa chama hicho ufutiliwe mbali.

Mkurugenzi wa tume ya TSC Nancy Macharia ameshikilia kuwa uhamisho utaendelea, kwani sera ya uhamisho ni sehemu ya kanuni na makubaliano baina yao.

Show More

Related Articles