HabariMilele FmSwahili

Raila kuongoza kampeni ya kumtafutia kura Ochilo Ayacko Migori leo

Kinara wa ODM Raila Odinga leo anazuru kaunti ya Migori ambako ataongoza kampeni ya kumtafutia kura mgombea wa useneta kaunti hiyo Dkt Ochilo Ayacko. Raila atazindua kampeni kabambe eneo la Rongo saa nne asubuhi kabla ya kuelekea Awendo  na kisa Uriri.Pia atahutubia mkutano wa hadhara huko Nyatike. anatarajiwa kurejelea wito wake kwa wakazi kujiepusha na watu anaosema wanalenga kuvuruga azma ya ODM kuhakikisha uwakilishi bora wa kaunti hiyo katika bunge la seneti.

Show More

Related Articles