HabariMilele FmSwahili

Baadhi ya viongozi wa Jubilee wazidi kupinga pendekezo la mageuzi ya katiba

Baadhi ya viongozi wa Jubilee wanazidi kupinga pendekezo la kuandaliwa kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba. Seneta wa Nakuru Susan Kihika anasema taifa lilitumia fedha nyingi kuandaa chaguzi mbili mwaka jana na kuwa haitakuwa vyema kwa wananchi kurejea debeni kwa sasa. Awataka wanasiasa kukomesha wito huo badala yake washirikiane katika kusaka mbinu za kuwaondolea wananchi mzigo wa gharama ya juu ya maisha.

Show More

Related Articles