HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta na naibu wake wamwomboleza mwanamuziki Joseph Kamaru

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ni baadhi ya viongozi ambao wamemwomboleza mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Kikuyu Joseph Kamaru.Kupitia kurasa zao za Twitter,viongozi hao wamemtaja Kamaru kama mwanamziki aliyetumia mziki wake kuhubiri umoja na amani miongoni mwa wakenya.Wengine waliomwomboleza Kamaru anayekumbukwa kwa nyimbo zake kama vile ‘Ndari ya mwalimu’ iliyoangazia uhusiano wa walimu na wanafunzi na  ‘Tiga kuhenia igoti’ yaani usidanganye kwa mahakama,ni spika wa bunge la seneti Ken Lusaka.Lusaka amekumbuka jinsi alivyokua rafiki wa karibu wa Kamaru alipohudumu kama DC huko Murang’a.Kamaru amefariki usiku wa kuamkia leo akipokea matibabu katika hosipitali ya MP Shah hapa Nairobi.Mwanawe Stephen Maina alidhibitisha kifo cha babake aliyefariki akiwa na miaka 79.Alizaliwa mwaka wa 1936 huko Kangema kaunti ya Murang’a kisha akaingia ulingo wa mziki mwaka wa 1956.Haya ni mojawapo ya mazungumzo yake katika kipindi cha Churchil Show mwaka 2016.

Show More

Related Articles