HabariMilele FmSwahili

Watoto 2 wafariki baada ya kupigwa na radi Trans Mara usiku wa kuamkia leo

Watoto 2 wamefariki baada ya kupigwa na radi kijiji cha Mmarti, Trans Mara Magharibi usiku wa kuamkia leo. aidha watoto wengine 3 hawajulikani walipo kufuatia tukio hilo lililofuatia mvua kubwa inayonyesha eneo hilo. Waathirwa walikuwa ndani ya nyumba yao wakati wa mkasa huo. Ajuza na mwanamke mmoja wa umri wa makamo wanapokea matibabu katika hospitali ndogo ya Emarti baada yao kuzirai kutokana na mshtuko.

Show More

Related Articles