HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Waomboleza Kifo Cha Mwanamziki Kamaru.

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza wakenya kuomboleza kifo cha mwanamuziki mashuhuri Joseph Kamaru, akitaja kifo chake kama pigo kubwa kwa sekta ya muziki nchini.

Mwanamuziki huyo wa nyimbo za benga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya MP shah Nairobi, ambapo amekuwa akipokea matibabu tangu siku ya Jumatatu.

Kulingana na Mtoto wake Stephen Maina Kamaru  alifariki mwendo wa saa tatu usiku wa kuamkia leo baada ya kushindwa kupumua.

Kamaru amefariki akiwa na miaka 79 ,na alianza kuimba nyimbo zake mwaka wa 1956

Show More

Related Articles