HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu Kadhaa Waripotiwa Kujeruhiwa Vibaya Kwenye Ajali Ya Kibarani Mombasa.

Watu kadhaa wamepata majeraha mabaya kwenye ajali katika eneo la Kibarani iliyohusisha lori lililokuwa limebeba majani Chai likielekea eneo la Changamwe.

Kulingana na msimamizi wa masuala ya trafiki ukanda wa pwani Emmanuel Okanda ni kwamba lori hilo lilikosa breki na kugonga magari mengine manane.

Okanda amesema kuwa magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo sita yalikuwa matatu na mbili gari za kibinafsi.

Wakati huo huo Okanda amesema kuwa ni kutokana na msongamano wa magari katika eneo hilo uliosababisha magari hayo yote kuhusika katika ajali.

Afisa huyo ameongeza kusema kuwa tayari uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo huku akisema kuwa maafisa wanafuatilia kujua idadi kamali ya waliohusika kwenye ajali hiyo.

Show More

Related Articles