HabariMilele FmSwahili

Shule zitakazohusika na udanganyifu wa mitihani ya kitaifa kufungwa

Shule zitakazopatikana zikihusika na udangayifu wa mitihani ya kitaifa mwaka huu zitafungwa.Waziri wa elimu balozi Amina Mohamed amekariri onyo lililotolewa na katibu wake Belio Kipsang na mwenyekiti wa baraza la mitihani KNEC dhidi ya shule zilizobainika kuwa na njama ya kuiba mitihani hiyo.amina anasema wahusika watakaopatikana wakiwaonyesha wanafunzi mitihani hiyo nao watakamatwa na kufikishwa mahakamani, akizungumza baada ya mkao na wadua wanaohusika na maandalizi ya mtaala mpya wa elimu,waziri Amina ametangaza mtaala huo mpya utazinduliwa rasmi mwaka ujao ilivyoratibiwa.anasema majaribio ya mtaala huo yameashiria kuwa tayari kutekelezwa mtaala huo.

Show More

Related Articles