HabariMilele FmSwahili

Sicily Kariuki:Idadi kubwa ya dawa zinazouzwa nchini ni gushi

Idadi kubwa ya dawa zinazouzwa nchini ni gushi. Waziri wa afya Sicily Kariuki amekiri sekta ya dawa imejaa dosari chungu nzima hali inayochangia mianya ya uagizaji dawa zisizokuwa salama kwa matumizi. Aidha Kariuki amelalamikia maduka za dawa zimesimamiwa na watu wasiohitimu huku ameamrisha msako wa kuyafunga mara moja.Usemi wake umeridhiwa na mwenyekiti wa muungano wa wauzaji dawa Louis Machogu anayekiri biashara yao imeingiliwa na matapeli ambapo ni asilimia 6 tu ya wauzaji dawa wamehitimu na kwamba wengine wanauza dawa bila leseni.Aidha, waziri Kariuki pia amesikitikia gharama ya juu ya dawa nchini akisema sera zinabuniwa kudhibiti bei hizo. Kuhusu  wizara yake kuwa miongoni mwa wizara fisadi nchini kwa mujibu wa EACC,Kariuki anasema anasubiri mapendekezo ya eacc kukabili zogo hilo katika wizara yake.

Show More

Related Articles