HabariMilele FmSwahili

Wabunge watofautiana kuhusu pendekezo la kubadilishwa tarehe ya uchaguzi

Wabunge wametofautiana kuhusiana na hoja ya kubadilishwa tarehe ya uchaguzi mkuu kutoka mwezi Agosti kila baada ya miaka mitano hadi mwezi Disemba.Hoja hiyo iliwasilishwa na mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa akielezea kwamba kuandaliwa uchaguzi mwezi Agosti kunaathiri maandalizi ya mitihani ya kitaifa na pia kusomwa bajeti ya taifa.Huku akirejelea jinsi hoja hiyo ilitupiliwa mbali na bunge la 11, Wamalwa amewataka wabunge kukubali hoja yake kwa manufaa ya wakenya wote.Wengi wa wabunge waliohudhuria kikao cha asubuhi ya leo wameelezea hisia kinzani baadhi wakiunga mkono kubadilishwa tarehe hiyo wengine wakitaka isalie ilivyo wakati huu.Hata hivyo wabunge hawakuruhusiwa kupiga kura kukubali au kupinga hoja hiyo baada ya kiranja wa wengi Benjamin washiali kusema wengi wa wabunge hawakuwa bungeni hivyo zoezi la kupiga kura lihairishwe.

Show More

Related Articles