HabariMilele FmSwahili

Mvulana wa miaka 8 akatwa mguu Makueni kwa kukosa huduma za matibabu

Mvulana wa miaka nane amelazimika kukatwa mguu wa kulia baada ya kudaiwa kukosa huduma za dharura katika kliniki moja ya kibinafsi huko Kilome kaunti ya Makueni. Inaarifiwa mvulana huyo alilazwa katika hospitali hiyo kwa juma moja bila kuhudumiwa alipofikishwa baada ya kugongwa na gari ambalo pia lilimuaa babake. Akidhibitisha kisa hiki waziri wa afya kaunti ya Makaueni Dkt Andrew Mutava  Mulwa amewalaumu maafisa kwenye kliniki hiyo kwa kufeli kumhudumia vyema kijana huyo kwa  muda hali iliyompelekea kukatwa mguu uliokuwa umeoza.Amesema maafisa wa umma mjini Makueni wameanzisha uchunguzi kwa lengo la kuwachukulia hatua wahudumu wa kliniki hiyo.

Show More

Related Articles