HabariPilipili FmPilipili FM News

Jamaa Akamatwa Kwa Kumbaka Nyanyake Makueni.

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 24 amekamatwa na polisi kaunti ya Makueni kwa tuhuma za kumbaka nyanyake mwenye umri wa miaka 77 katika kijiji cha Utangwa , eneo la Mbooni.

Kamanda wa polisi kaunti ya Makueni Joseph Nepeiyan anasema kijana huyo ametiwa mbaroni baada ya kupatikana akitekeleza kitendo hicho katika makazi ya mwathiriwa.

Nyanyake kijana huyo amesafirishwa hadi hospitali ya wanawake ya Nairobi kupokea matibabu.

Visa vya ubakaji kaunti ya makueni vimetajwa kuongezeka siku za hkaribuni kulingana na naibu gavana wa kaunti hiyo Andelina Mwau.

Show More

Related Articles