HabariPilipili FmPilipili FM News

Aukot Apinga IEBC Kuvunjiliwa Mbali.

Wito umetolewa kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC kuufanyia mabadiliko mfumo wake wa kuandikisha wapiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Akiongea mda mfupi baada ya kufanya mkutano na maafisa wa tume hiyo, mwenyekiti wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot, amesema ipo haja ya tume hiyo kutumia kitambulisho cha kitaifa kama stakabadhi ya msingi kusajili wapiga kura.

Aukot amepinga kauli za baadhi ya wanasiasa wanaotaka tume hiyo ivunjiliwe mbali, akisema makamishna waliokiuka matakwa ya utendakazi wao ndio wanaopaswa kuadhibiwa.

Show More

Related Articles