HabariMilele FmSwahili

Naibu spika wa seneti Kithure Kindiki aunga mkono mageuzi ya katiba

 

Naibu spika wa seneti Kithure Kindiki anashikilia taifa linahitaji mageuzi katiba. Hata hivyo Kindiki anaonya mageuzi hayo hayafai kuwatafutia watu fulani nyadhfa za uongozi.Nalo,kundi la waliokua wabunge wa zamani linaunga mkono mageuzi hayo ya kikatiba.Wakiongea baada ya mkao wa faragha hapa Nairobi,wabunge hao wanataka baadhi ya nyadhfa serikalini kufutiliwa mbali.Na akizungumza baada ya kukutana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, kiongozi wa chama cha Third Way Alliance Dkt Ekuru Aukot sasa anadai IEBC imeridhia ombi lake la kuandaliwa kura ya maoni ili kuifanyia mageuzi katiba. Aukot anasema IEBC imeahidi kwamba kupitia kamati yake maalum ya kuangazia masuala ya kura ya maoni inatathmini mapendekezo yake.

Show More

Related Articles