HabariMilele FmSwahili

Duka litakalouza unga wa ugali wa kilo 2 kwa zaidi ya 75 Nairobi kufungwa

Duka litakalouza unga wa ugali wa kilo 2 kwa zaidi ya shilingi 75 kaunti ya Nairobi litafungwa.Ndilo onyo la gavana Mike Mbuvi Sonko anayesema ni sharti agizo la serikali kutiliwa maanani na wafanyibiashara.Kupitia waziri wa biashara Nairobi,Sonko anasema hatosalia kimya huku wenyeji wa kaunti wakiendelea kulaghaiwa .Serikali juma jana ilitangaza bei hiyo ya shilingi 75 kuwa rasmi baada ya kukubaliana na wasaga nafaka nchini.

Show More

Related Articles