HabariMilele FmSwahili

Wapambe wa Ruto wazidi kumshutumu Raila kwa kutaka kuvuruga Jubilee

Viongozi wa Jubilee wanaoegemea upande wa naibu rais William Ruto wameendelea kumshutumu kinara wa ODM Raila Odinga kwa madai ya kupanga njama ya kumpaka tope naibu rais Ruto. Kulingana na mbunge wa Kimilili Didmus Barasa Raila amekuwa akitumia changamoto zinazokumba taifa kumhujumu Ruto. Amepinga vikali madai kuwa naibu rais alipanga vurugu zilizoshuhudiwa bungeni wakati wa vikao vya kupasisha sheria ya fedha ya mwaka 2018.

Show More

Related Articles