HabariMilele FmSwahili

Dkt Ekuru Aukot ashauriana na IEBC kuhusu maandalizi ya kura ya maoni

Kiongozi wa chama cha Third Way Alliance Dkt Ekuru Aukot anasema tume ya uchaguzi IEBC imebuni kamati ya kuandaa kura ya inayoshinikizwa na chama hicho. Akizungumza katika makao makuu ya IEBC Dkt Aukot anasema mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukhati amemhakikishia kuwa tayari kwa zoezi hilo. Kati ya mengine Aukot anataka katiba kufanyiwa mabadiliko ili kupunguza idadi ya wabunge hadi 194.Kadhalika anasema Chebhukati amemhakikishia kuwa makamishna wa IEBC wanaohusishwa na matumizi mabaya ya fedha za tume hiyo wanaandamwa na mamlaka husika ikiwemo afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Show More

Related Articles