HabariPilipili FmPilipili FM News

Pesa Bandia Zanaswa Nairobi.

 

Mkenya mmoja  na raia wawili wa kigeni wanazuiliwa na polisi Jijini Nairobi, baada ya kupatikana na shilingi bilioni moja pesa bandia .

Watatu hao walikamatwa katika makazi ya sandal Wood eneo la westlands huko Nairobi.

Kupitia mtandao wa twitter idara ya upelelezi wa jinai DCI imemtambua mkenya aliyekamatwa kama Antony Mwangangi na  raia wawili wa taifa la Chad kama Abdalla Tamba na mtoto wake Abdoulaye.

Watatu hao walikamatwa na kikosi cha maafisa wa flying squad, baada ya kupashwa habari na wananchi.

Dolla Feki za kimarekani, Euro pamoja na pesa za Kenya ni kati ya pesa zilizonaswa.

Show More

Related Articles