HabariMilele FmSwahili

Rais apongeza zoezi la unadhifishaji jiji la Nairobi linaloongozwa na Sonko

Rais Uhuru Kenyatta amepongeza zoezi la unadhifishaji jiji la Nairobi linaloongozwa na gavana Mike Sonko. Rais Kenyatta ameelezea kuridhishwa na zoezi hilo ambalo lilianzishwa miezi mitatu iliyopita katika wadi 85 hapa jijini. Kadhalika rais Kenyatta ameridhia ombi la gavana Sonko la kuhudhuria usafishaji wa eneo la Kasarani jumamosi hii na kilele cha usafisahi jiji katika uwanja wa Maji Mazuri. Amempongeza gavana Sonko kwa kuwahusishavijana katika mpango huo.

Show More

Related Articles