HabariMilele FmSwahili

Serikali yakanusha madai ya kumpa huduma tofauti na wafungwa wengine Obado

Serikali imekanusha madai ya kumpa huduma tofauti na wafungwa wengine gavana wa Migori Okoth Obado.Katika taarifa kwa vyombo vya habari kamishna wa magereza Isiah Osugo anasema Obado anakula, kulala na kuvaa kama wafungwa wengine.Kadhalika Osugo anasema gavana huyo anayekabiliwa na kesi ya mauaji anaruhusiwa tuu kuvaa nguo zake binafsi anapofikishwa mahakamani.Obado ni miongoni mwa wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Sharon Otieno ambaye alikuwa mpenziye.

Show More

Related Articles