HabariPilipili FmPilipili FM News

Fisi Awavamia Punda Katika Kaunti Ya Lamu.

Daktari mkuu wa masuala ya  punda  kaunti ya Lamu Felix Rachuonyo amewasihi wakaazi wa Lamu kuwalinda punda wao ili wasivamiwe na fisi, kwani punda ni mnyama mwenye thamani kubwa kaunti hiyo haswa katika shughuli za ubebaji wa bidhaa.

Hii ni baada ya zaidi ya punda 50 kushambliwa na kuliwa na fisi katika maeneo mbali mbali ya Lamu ikiwemo Kipungani,mji wa Lamu,Matondoni,Kihobe, Kizingitini,Siyu, na  Tchundwa.

Katika kikao na waandishi wa habari Rachuonyo amehimiza shirika la wanyama pori KWS kuharakisha ili kumkamata fisi huyo na kumrudishwa msituni kwani anapelekea hasara kubwa kwa wakaazi sawia na kuwatishia maisha yao.

Show More

Related Articles