HabariPilipili FmPilipili FM News

Kituo cha CT SCAN cha zinduliwa Mjini Voi Katika Kaunti Ya Taita Taveta.

Naibu wa rais William Ruto hii leo amezindua kituo kipya cha CT scan  atika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi.

Ruto amesema kituo hicho cha kisasa kilichoigharimu serikali shilingi millioni mia moja kinatarajiwa kutoa huduma za picha kwa mamia ya wagonjwa ambao wamekuwa wakisafiri safari za mbali hadi Mombasa na Nairobi kupata huduma hiyo.

Naibu rais amesema serikali ya kitaifa inashirikiana na serikali za kaunti katika azma ya kuboresha afya  ya mwananchi kote nchini.

Ruto pia anatarajiwa kuzindua miradi kadha ya maendeleo katika kaunti hiyo huku akitamatisha ziara yake katika ukanda wa Pwani hii leo.

Show More

Related Articles