HabariMilele FmSwahili

Ruto azidi kumkosoa Odinga kwa kujaribu kutatiza amani Jubilee

Naibu rais William Ruto amepuuzilia mbali shutuma dhidi yake zinazoelekezwa na wanasiasa wa upinzani. Akizungumza mjini Voi kaunti ya Taita Taveta, naibu rais amewasuta viongozi wa chama cha ODM kwa kushutumu matamshi yake kuhusiana na kinara wa ODM Raila Odinga. Amewatuhumu viongozi hao kwa kukosa agenda maalum kwa taifa huku akiapa kuendelea kumshutumu Raila kwa madai ya kupanga njama ya kuvuruga udhabiti ndani ya chama cha Jubilee.Ruto ambaye  amezindua miradi kadhaa ya maendeleo mjini Voi ikiwemo chumba cha CT Scan katika hospitali ya Moi  amewataka wakazi wa Taita Taveta kushirikiana na serikali ya Jubilee katika kufanikisha miradi ya maendeleo. Amewataka kujitenga na upinzani anaosema unalenga kupanda mbegu ya migawanyiko miongoni mwa wakenya.

Show More

Related Articles