HabariMilele FmSwahili

Idara ya polisi ndio inaongoza kwa ufisadi,utafiti wa tume ya ufisadi EACC wabaini

Wizara ya usalama wa ndani ndio fisadi zaidi nchini ikiwa na asilimia 64. Utafiti wa tume ya EACC unaonyesha wizara ya pili fisadi ni ile ya afya kwa asilimia 27.8 huku ya ardhi ikiwa ya tatu kwa asilimia 23.9.Afisa mkuu mtendaji wa EACC Halakhe Waqo, hata hivyo anasema idadi ya wakenya wanaotoa hongo ili kupata huduma kutoka afisi za serikali imepungua hadi asilimia 38.9.Aidha Waqo anasema kwa mwaka mmoja EACC imefanikiwa kuokoa shilingi milioni 500 zilizokuwa zimeporwa kwa njia  za ufisadi.Mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukhala aidha ameelezea haja ya kukaguliwa kila mwaka maafisa wa umma pamoja na kufanyiwa marekebisho ya kina sheria za kukabili ufisadi nchini

Show More

Related Articles