HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Usalama Wa Ndani Yatajwa Kuwa Fisadi Zaidi Hapa Nchini.

Wizara ya usalama wa ndani imeorodheshwa kuwa fisadi zaidi nchini kwa asilimia 64, ikifuatiwa na wizara ya afya pamoja na ile ya ardhi.

Ripoti ya uchunguzi ya hivi karibuni inaonyesha kuwa Idara ya polisi ni fisadi kwa asilimia 23.8 , ikifuatiwa na tume ya huduma kwa polisi NPSC kwa asilimia 13.7.

Aidha kulingana na utafiti uliofanywa kati ya September 18 na octoober 24 mwaka jana na kuwahusisha wakenya 5,977 ndani ya kaunti zote 47, asilimia 76 ya wakenya wanadai hawawezi kupata huduma za serikali bila kutoa hongo.

Show More

Related Articles