HabariPilipili FmPilipili FM News

Maribe Kuzuiliwa Kwa Siku 10.

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe ataendelea kuzuiliwa kwa siku kumi zaidi ili kupisha upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi wao dhidi yake.

Akitoa uamuzi huo hakimu mkuu  wa mahakama ya Kiambu  Justus Kituku amesema ipo haja ya upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi wao dhidi ya mshukiwa huyo.

Awali upande wa mashtaka ulikua umeomba siku 14 huku wakili wa Maribe Katwa Kigen akitaka mteja wake kuzuiliwa kwa siku tatu kabla ya kurudishwa mahakamani lakini ombi hilo limepingwa vikali na upande wa mashtaka.

Maribe amefikishwa mahakamani akiwa anahusishwa na mauaji ya Monica Kimani, ambapo gari lake linadaiwa lilitumiwa na mpenziwe Joseph Irungu usiku wakufariki kwa Monica.

Irungu tayari wiki iliyopita alifikishwa mahakamani na anaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

Tayari makachero wa serikali wanaendeleza uchunguzi wa chembechembe za DNA kwa mabaki ya nguo zilizopatikana kubaini kama zilikua za Irungu au la.

Maribe atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri huku wakili wake akipewa ruhusa yakumtembelea kituoni humo.

Show More

Related Articles