HabariMilele FmSwahili

Jacque Maribe kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gilgil kwa siku 10

Mwanahabari Jacque Maribe atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Gilgil kwa siku 10 wakati uchunguzi kuhusu kifo cha Monica Kimani unaendelea.Hakimu mkuu wa mahakama ya Kiambu, anasema uzito wa kesi hiyo umempa sababu za kuupa upande wa mashtaka muda zaidi kumchunguza mwanahabari huyo.Aidha hakimu huyo amewataka polisi kuwaruhusu mawakili wa Maribe kutangamana na mteja wao wakati atakuwa anazuiliwa

Show More

Related Articles