K24 TvNEWSSwahiliVideos

UHAYAWANI WA ‘EMBAKASI RANCH’: Mwanamke avamiwa na kukatwa katwa kwa panga na majembe

Huku serikali ikiendelea kutafuta njia za kutatua mzozo unaoikumba kampuni ya mashamba ya Embakasi Ranch, eneo la Embakasi Nairobi, mwanamke mmoja anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 70 alivamiwa na kukatwa katwa kwa mapanga na majembe na watu anaowafahamu.

Inasemekana mwanamke huyo kwa jina Josephine Gakami alikuwa amelala nyumbani kwake siku ya Alhamisi wakati watu hao walipomvamia.

Inaaminika mama huyo ambaye hali yake kufikia sasa haijulikani alishambuliwa kuhusiana mgogoro wa umiliki wa vipande viwili vya shamba eneo hilo la Embakasi.

Show More

Related Articles