HabariPilipili FmPilipili FM News

KRA Yaondoa Ushuru Wa Bidhaa Ambazo Zimekaa Sana Bandarini.

Halmashauri ya bandari nchini pamoja na halmashauri ya ukusanyaji ushuru KRA, imetangaza kuondolewa kwa ada za malimbikizo kwa bidhaa na makasha ya wateja  ambayo yamekaa katika bandari ya Mombasa na hifadhi ya makasha ya Nairobi kwa zaidi ya muda wa siku ishirini na moja kinyume cha sheria.

Haya ni kulingana na tangazo kwa umma kutoka kwa meneja wa KPA na kamishna  Mkuu wa KRA.

Wateja hao wanatarajiwa kuondoa mizigo yoa katika muda wa siku kumi na nne kuanzia leo.

Kupitia chapisho hilo mamlaka ya KPA na KRA,  pia imetoa onyo kuwa bidhaa zitakazo kosa kuondolewa kwenye bandari ya Mombasa, na hifadhi ya makasha Nairobi katika muda uliowekwa, zitapigwa mnada au kuharibiwa kulingana na kipengee cha usimamizi kutoka jumuiya ya usimamizi wa forodha Afrika Mashariki.

Show More

Related Articles