HabariMilele FmSwahili

Ibada ya misa ya wafu ya Monica Kimani yaendelea Thika

Ibada ya wafu ya Monica Kimani aliyeuwawa katika njia tatanishi mtaani Kilimani mapema juma hili hapa Nairobi inaandaliwa wakati huu katika uwanja wa chuo kikuu cha M.K.U Thika. Familia, jamaa na marafiki wanaohudhuria ibada hiyo wamemtaja Monica kama msichana mcha Mungu ambaye kufariki kwake akiwa mchanga kumewapokonya msichana jasiri. Mjombake Monica John Nganga akitaka haki kwa familia.Mmoja wa marafiki wa karibu wa familia ya Monica, anasema mazungumzo yao ya mwisho na Monica ilikuwa jinsi alitaka kusheherehea siku yake ya kuzaliwa kwake Oktoba 10 kwa njia ya kipekee

Show More

Related Articles