HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanasiasa Wanaotoa Matamshi Ya Chuki Haswaa Mitandaoni Wameonya Vikali.

 

Mkurugenzi wa tume ya uwiano na utangamamo wa kitaifa NCIC Hassan Mohammed amesema hawatakubali viongozi kutoa matamshi ya chuki ambayo huenda yakaleta vurugu.

Amesema siasa za chuki zilikwisha wakati rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga walipoungana kupitia handshake, hivyo kuwataka wanasiasa kukoma kutumia visa vya mizozo ya mifugo, mipaka na kufurushwa kwa watu kutoka msitu wa Mau kwa kuingiza siasa.

Ameongea haya wakati wa mkutano uliojumuisha washikadau na makamishna kadhaa wa kaunti wa kuwahamasiha kuhusiana na masuala ya uwiano na amani wakati wa uchaguzi ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kura zinaandaliwa kwa amani

Show More

Related Articles