HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Waombwa Kujiunga Na Vyuo Vya Mafunzo Ya Ubaharia.

Halmashauri ya ubaharia nchini KMA imehimiza vijana kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ubaharia.

Akiongea kwenye hafla ya kusherehekea siku ya ubaharia katika ukumbi wa mama ngina kaunti ya Mombasa mkurugenzi mkuu wa halimashauri hio George Macgoye amesema sasa somo la ubaharia limeanza kufunzwa katika vyuo vikuu mbali mbali nchini.

Kuhusiana na usalama wa baharini Macgoye amesema kwa sasa hali ya usalama katika bahari ya Kenya iko sawa na wamewekeza katika tekinolojia ya mawasiliano kutambua aina yoyote ya hatari.

Show More

Related Articles