HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Waombwa Kujitokeza Kufanyiwa Ukaguzi Wa Maradhi Ya Figo.

Bei ghali ya dawa kwa wagonjwa wa figo  imetajwa kuwa  changamoto kuu inayowakumba waathiriwa  wa Ugonjwa huo hususan wale waliobandikwa figo

Baadhi ya waathiriwa wameomba shirika la bima ya afya nchini NHIF  kuingilia kati kuwafadhili  ili kupunguza gharama za juu za dawa hizo, ambazo wanazihitaji ili kuimarisha afya zao.

Yakijiri hayo wakenya wameombwa kujitokeza kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini iwapo wamo kwenye hatari ya kuathirika na ugonjwa huu  ili kupata huduma za matibabu kwa mapema tena bei ya nafuu.

Haya wamezungumzwa na madakitari pamoja na wataalam wa magonjwa ya figo katika kongamano la 15  la kisayansi linaloendelea katika hoteli moja hapa mjini mombasa.

Show More

Related Articles