HabariMilele FmSwahili

Obado kurejea kizimbani leo kufahamu hatma yake

Gavana wa Migori Okoth Obado anarejea kizimbani leo kufahamu hatma yake iwapo ataachiliwa kwa dhamama au la katika kesi ya mauaji ya Sharon Otieno. Jaji Jessi Lesit atatoa uamuzi wake baada ya Obado kukanusha mashtaka na kuomba kuachiliwa kwa dhamana kesi hiyo ikiendelea. Upande wa  ukiongozwa na  naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Jacob Ondari unaitaka mahakama kuamuru Obado kusalia kizuizini kutokana na uzito wa mashtaka yanayomkabili.

Show More

Related Articles