People Daily

Mikakati Kabambe Yawekwa Ilikuimarisha Usalama Katika Bandari Ya Mombasa.

Mikakati imewekwa kuhakikisha hakuna makasha ambayo yataibwa au kupitishwa bila ya kukaguliwa katika bandari ya Mombasa na kwenye hifadhi ya makasha eneo la Embakasi jijini Nairobi.

Mkurugenzi mkuu wa oparesheni ya shughuli za bandari nahodha William Rutto amekiri kuwepo wizi wa makasha,jambo ambalo anadai wanalifanyia kazi ili kuziba mianya yote inayotumiwa na mawakala na baadhi ya maafisa wa mashirika ya serikali.

Rutto amebaini mchakato wa kuziba mianya ya wizi na uingizaji wa bidhaa ghushi imechangia kucheleweshwa kwa makasha kufika embakasi kwa wakati ufaao.

Show More

Related Articles